Mbunge wa Kawe jijini Dar es salaam Halima Mdee amemkaribisha aliyekuwa
Mbunge wa Singida Kaskazini ndani ya chama chao huku akimtahadharisha
kuhusu changamoto wanazokumbana nazo viongozi wa chama hicho.
Halima Mdee ame
tumia mtandao wake wa kijamii wa Twitter kumkaribisha
Nyalandu ambaye leo ametangaza kujiuzulu nafasi zake za uongozi ndani ya
Chama Cha Mapinduzi pamoja na nafasi yake ya ubunge aliokuwa nao.
"Mhe. Nyalandu karibu sana CHADEMA. Naamini utakuwa imara kukabiliana
na siasa za chuki, ubaguzi na visasi zinazolikabili taifa letu".
Mapema leo Mh. Nyalandu ambaye alikuwa Mbunge wa Singida Kaskazini na
Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM litangaza kujiuzulu nafasi zake hizo kwa
kile alichodai kwamba hafurahishwa na mambo ya kisiasa yanayoendelea
nchini na kuwaomba wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo kama
wataridhia wampe nafasi ili kuweza kuleta mabadiliko ya kisiasa na
kiuchumi kupitia chama hicho.


8:53 AM
0 comments:
Post a Comment