Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini Mh. Zitto
Kabwe, amekamatwa na Jeshi la Polisi asubuhi hii akiwa nyumbani kwake
jijini Dar es salaam na
amepelekwa kituo cha Polisi Chang'ombe.
Taarifa fupi iliyotolewa na Afisa habari wa Chama hicho Abdallah Khamis, amethibitisha kukamatwa kwa kiongozi huyo huku akibainisha kwamba sababu za kukamatwa kwake zinawezekana kuwa ni kutokana na hotuba yake aliyoitoa juzi Oktoba 29, 2017 katika kata ya Kijichi, Mbagala Jijini Dar es salaam katika uzinduzi wa kampeni za uchaguzi wa mdogo wa madiwani kwenye kata 43 nchini.

11:15 PM
0 comments:
Post a Comment