skip to main |
skip to sidebar
Na Mwandishi wetu.
Balozi Gomile-Chidyaonga alifariki ghafla Ijumaa iliyopita na mwili
wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.imesemekana kuwa
Chanzo cha kifo cha Balozi wa Malawi nchini, Flossy Gomile-Chidyaonga
kimefahamika. Uchunguzi wa madaktari umebaini kuwa kilitokana na moyo
wake kushindwa kufanya kazi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, John Haule alisema jana kuwa taarifa za
madaktari zinaonyesha kuwa mshipa mkubwa wa moyo wake ulipasuka na
kusababisha kifo chake.
“Jana (juzi) madaktari waliufanyia
uchunguzi mwili wake (postmortem) na kubaini kuwa mshipa mkubwa wa moyo
ulipasuka na kutiririsha damu nyingi mwilini hali iliyosababisha kifo
chake,” alisema Haule.
Haule alisema Serikali ilikuwa karibu na
familia ya marehemu tangu ilipopata taarifa ya kuzidiwa kwake na
ilishirikiana vyema na ndugu na jamaa kumpeleka katika Hospitali ya Aga
Khan na hatimaye Muhimbili.
“Kesho (jana Jumatatu) kati ya saa
3:30 na saa 4:00 asubuhi itafanyika misa ya kumwombea katika Ukumbi wa
Mwalimu Julius Nyerere pia heshima za mwisho zitatolewa hapo.
Baadaye mwili wa marehemu utapelekwa Uwanja wa Ndege kwa ajili ya safari ya kwenda Malawi Jumanne,” alisema.
Marehemu
anatarajiwa kuzikwa nyumbani kwake huko Blantyre, Jumatano na Haule
alisema Serikali ya Tanzania itashiriki kikamilifu katika tukio hilo.
Juzi, Rais Jakaya Kikwete alimtumia salamu za rambirambi Rais wa Malawi, Joyce Banda kutokana na msiba huo mkubwa.
Alisema
Balozi Gomile-Chidyaonga alikuwa kiungo muhimu katika kukuza uhusiano
baina ya Malawi na Tanzania na kwamba kifo chake kimeshtusha kwa kuwa
bado alikuwa anahitajika katika nchi hizo mbili.
“Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za msiba wa Balozi Gomile-Chidyaonga ni huzuni kwetu sote,” alisema.
Rais Kikwete.
huku
akimwomba Rais Banda amfikishie salamu zake na za Watanzania kwa jumla
kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa na Wamalawi wote.
Kabla ya
kuwa Balozi Tanzania, Gomile-Chidyaonga aliwahi kuwa Kaimu Balozi wa
Malawi nchini Uingereza kabla ya kumwondoa kutokana na mgogoro wa
kidiplomasia baina ya nchi hizo.
Marehemu pia aliwahi kuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Malawi.
0 comments:
Post a Comment