skip to main |
skip to sidebar
Na Mwandishi wetu.

Utafiti mpya umebaini kuwa Tanzania inapoteza zaidi ya Sh3 trilioni
kila mwaka kutokana na ukwepaji kodi unaofanywa na kampuni za uchimbaji
madini na katika uingizaji bidhaa na kuuza nje.
Shirika la
kiuchumi lenye makazi yake Marekani (GFI), lilitoa ripoti yake mwishoni
mwa wiki iliyopita likieleza kuwa Tanzania inaongoza kwa kupoteza fedha
nyingi zaidi kutokana na udanganyifu huo miongoni mwa nchi tano
zilizofanyiwa utafiti za Kenya, Uganda, Ghana na Msumbiji.
Kiasi cha fedha kinachopotea kila mwaka, kingeweza kujenga zahanati 374 za kisasa kwa Sh8.1 bilioni kila moja.
Vilevile,
utafiti huo umeonyesha kuwa kiasi hicho kinachopotea kingeweza
kulisaidia Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), kuzalisha nishati ya
kiasi cha megawati 1,800, tatizo ambalo limekuwa sugu kwa miongo mingi.
Pia,
kiasi hicho kingeliwezesha Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kununua
ndege 30 aina ya A320 ambayo hugharimu dola 60 milioni kila moja. Hivi
karibuni Shirika la Ndege la Afrika Kusini lilinunua ndege hiyo.
Udanganyifu katika mauzo ulionekana zaidi katika uingizaji mafuta yenye msamaha wa kodi kwa kampuni za madini.
Ripoti
hiyo inaonyesha kuwa huenda kampuni za madini hupandisha gharama za
uingizaji wa nishati hiyo ili kuhamisha fedha nje ya nchi kwa njia
haramu.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, kiwango ambacho Tanzania hupoteza kila mwaka ni sawa na asilimia 16 ya bajeti ya sasa.
Utafiti
huo pia unaonyesha kuwa kiasi kinachopotea ni mara tatu ya kile ambacho
Serikali ilitangaza kukopa kupitia mashirika ya mikopo yenye masharti
nafuu katika bajeti yake ya sasa.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo,
Tanzania inafuatiwa na Kenya ambayo inapoteza Sh131 bilioni za Kenya
(Sh2.489 trilioni), Ghana Dola za Marekani 1.44 bilioni (Sh2.304
trilioni) na Uganda Sh2.2 trilioni za Uganda (Sh1.4 trilioni) na
Msumbiji iliyopoteza Dola za Marekani 585 milioni (Sh936 bilioni).
0 comments:
Post a Comment