skip to main |
skip to sidebar
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Raymond Mushi, amewataka
viongozi wa elimu pamoja na wamiliki wa shule nchini kuwa na utaratibu
wa kufanya tathimini za mara kwa mara katika shule, ili kutafakari njia
za kutoa elimu bora kwa wanafunzi.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mushi , alitoa rai hiyo jijini Dar es Salaam
jana wakati wa kutoa tuzo ya vyeti kwa shule za msingi na sekondari
pamoja na wanafunzi waliofanya vizuri katika Mkoa wa Dar es Salaam
katika kuadhimisha Wiki ya Elimu.
Alisema wamiliki wa shule na wadau wana dhima kubwa katika
kukomboa elimu na kuhakikisha wanafikia malengo ya Matokeo Makubwa Sasa
(BRN).
Alizipongeza shule zilioibuka kidedea katika mitihani ya mwaka
jana ambazo ni Tusiime na St. Joseph Millenium kutoka Wilaya ya Ilala
ambayo ilipata wastani wa 230, Montfort (Temeke) na Fountain of Joy
(Kinondoni).
Shule nyigine ni Hazina (Kinondoni), Nyiwa, Heritage na New Ambasador (Ilala), Holy Cross (Temeke) na Anazak (Kinondoni).
“Kwa
upande wa shule zetu za serikali tumejitahidi kidogo ambapo naipongeza
Zanaki, Msimbazi Mseto, Msimbazi, Boma zote kutoka Ilala, Kijitonyama
Kisiwani, Mirambo na Mapambano (Kinondoni), Maktaba, Umoja wa Mataifa,
Mkoani (IIala),” alisema Mushi.
Sekondari zisizo za kiserikali zilizofanya vizuri ni Thomas More
Machrina, Feza Girl, Canossa, Alpha, Feza Boys, Hellen’s, St. Joseph
Millennium, Rising Star na Barbro Johansson zote kutoka Wilaya ya
Kinondoni pamoja na Tusiime ya Ilala.
“Shule za serikali zilizofanya vizuri ni Jangwani, Zanaki,
Benjamin William Mkapa (Ilala), Chang’ombe, Kibasila (Temeke), Pugu,
Azania, Kisutu Dar es Salaam (Ilala) pamoja na Kiluvya Kinondoni,”
alisema Mushi.
Alieleza changamoto zinazoikabili sekta ya elimu kuwa ni upungufu
wa shule za sekondari, upungufu wa walimu masomo ya Hisabati na
Sayansi, uchakavu wa miundombinu pamoja na ufaulu wa chini wa wanafunzi
wanaohitimu mafunzo katika ngazi mbalimbali.
“Kuna upungufu wa vyumba vya madarasa 4,314 kwa sekondari,
matundu ya vyoo 16,046, na madawati 76,029. Kwa upande wa shule za
msingi kuna upungufu wa madarasa 1,020, matundu ya vyoo 3,531 na
madawati 35,420 kwa shule za serikali za sekondari,” alisema.
0 comments:
Post a Comment