Saturday, May 10, 2014

LUDOVICK UTOUH AZINYOOSHEA KIDOLE TDFA

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh (katikati) akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika bungeni, mjini Dodoma juzi. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (Laac), Rajab Mbarouk Mohammed

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), amezinyooshea kidole mamlaka mbili za Serikali kwa kushindwa kudhibiti uingizaji wa bidhaa zisizo na ubora nchini.


CAG imetoa taarifa kuhusu ukaguzi wa ufanisi na ukaguzi maalumu kwa kipindi kinachoishia Machi 31, 2014, imezitaja taasisi hizo kuwa ni Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA), akisema zilipwaya katika ukaguzi wa ubora wa chakula kinachoingizwa na kuzalishwa nchini.


Taarifa hiyo imebainisha kuwa ufuatiliaji ulishindwa kuzuia viwanda vya usindikaji chakula kuvunja sheria mara kwa mara.


Asilimia 80 ya viwanda vilivyokuwa vimekiuka sheria havikuchukuliwa hatua, huku kukiwapo makosa ya kujirudiarudia kwa wasindikaji na waagizaji chakula nje ya nchi. Kwa mujibu wa CAG.
Taarifa hiyo imesema kwa hali inavyoonekana, idadi ya bidhaa hafifu nchini imekuwa ikiongezeka kwa miaka mitatu kwa kati ya asilimia 30 na 40 kutoka mwaka wa fedha wa 2010/2011.
Bidhaa hizo nyingi hupita katika bandari na mipaka ya Tanzania ambayo wakaguzi wa TBS walitakiwa kuzikagua, lakini kutokana na upungufu wa ukaguzi, zimekuwa zikiingia nchini.
Taarifa hiyo, CAG alisema ukaguzi wa ubora wa bidhaa zinazoingia nchini haukufanyika vizuri na vya kutosha na ukaguzi wa bidhaa kutoka nje haukufanywa kwa kuzingatia viashiria hatarishi.
“Bidhaa zote zilipewa kipaumbele sawa wakati wa ukaguzi licha ya ukweli kwamba baadhi ya bidhaa zinajulikana kuwa na athari kubwa kwa afya na mazingira ya walaji nchini,” asema

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Powerade Coupons