skip to main |
skip to sidebar
Dodoma: Mbunge wa viti maalumu kwa tiketi ya Chadema, Susan Lyimo jama alidai kuwa msongamano wa magri jijini Dar es salaam sasa umeanza kuibua migogoro ya ndoa katika familia.
Susan alisababisha wabunge wenzake kuangua kicheko wakati alipotoa kauli hiyo akichangia hotuba ya bajeti ya ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka 2014/2015.
Mbunge huyo alisema ingawa wanaume wa Dar es salaam wanatoka kazini saa 11:00 jioni, wamekuwa wakifika majumbani mwao saa 6:00 usiku kwa kisingizio cha msongamano wa magri kutoka maeneo yao ya kazini.
"Mimi ni mtaalamu wa saikolojia nimekuwa nikipata kesi nyingi sana za ndoa. Sasa hivi wanaume hawarudi mapema nyumbani kwa sababu ya msongamano.Wanatoka kazini saa 11:00 na kufika saa 6:00 usiku" alisema.
" Ka kuona foleni zipungue wanaamua kwenda kwenye mabaa ili folen zipungue waanze safari ya kurudi nyumbani saa 5:00 usiku.
Tunaomba Waziri Mkuu barabara hizi zitengenezwe ili kunusuru ndoa hizi.Susan aliendelea kuwavunja mbavu wabunge wa Bunge la Muungano pale aliposema "Hata sasa hivi tunaona watooto wasiokuwa na wazazi wanakuwa wengi kutokana na msongamano wa magari. Tunaomba sana waziri mkuu kuhakikisha tatizo hili linatatuliwa kwa sababu ni janga la kitaifa.
Alisema pamoja na nia nzuri ya kutoa fedha kujenga kwa ajili ya ujenzi wa barabara za lami jijini Dar es salaam,barabara nyingi zinajengwa chini ya kiwango.
0 comments:
Post a Comment