skip to main |
skip to sidebar
Taasisi ya RafikiElimu Foundation kupitia MRADI WA WANAWAKE SALAMA
TANZANIA inatangaza nafasi za mafunzo ya UANDAAJI NA UTENGENEZAJI WA
VYAKULA-LISHE MAALUMU KWA WAGONJWA NA WENYE MATATIZO MBALIMBALI YA
KIAFYA.
Wahitimu wa mafunzo haya watapata nafasi ya kufanya kazi kama waandaji
na watayarishaji wa Vyakula –Lishe katika MRADI WA WANAWAKE SALAMA
TANZANIA.
Masomo yatakayo tolewa ni pamoja na UANDAAJI WA VYAKULA-LISHE MBALIMBALI pamoja na AFYA YA UZAZI KWA WANAWAKE.
SIFA ZA MWOMBAJI NAFASI.
1. Awe wa jinsia ya kike.
2. Awe na elimu ya kuanzia kidato cha nne na kuendelea.
3. Awe anaishi jijini Dar Es salaam.
4. Awe tayari kufanya kazi kama muandaaji na mtayarishaji wa vyakula-lishe katika MRADI WA WANAWAKE SALAMA TANZANIA.
5. Awe na uwezo wa kusoma na kuelewa mwenyewe kwa njia ya vitabu na VIDEO CD bila kuingia darasani.
KUANZA KWA MAFUNZO : Mafunzo haya taanza tarehe 21 JULAI 2014.
MUDA WA MAFUNZO :
Mafunzo haya yatafanyika kwa muda wa mwezi mmoja .
ADA YA MAFUNZO :
Mafunzo haya yanatolewa BURE chini ya udhamini wa mashirika hisani..
FOMU ZA KUJIUNGA NA MAFUNZO :
Fomu za kujiunga na mafunzo haya zinapatikana katika ofisi zetu
zilizopo katika eneo la CHANGANYIKENI karibu na CHUO CHA TAKWIMU mbele
ya CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM.
JINSI YA KUFIKA OFISINI KWETU :
Panda daladala za UBUNGO-CHANGANYIKENI kasha shuka kituo cha TAKWIMU
halafu tembea hatua ishirini mbele kasha tazama upande wako wa kulia
utaona ofisi imeandikwa RAEFO TANZANIA.
MWISHO WA KUCHUKUA FOMU:
Mwisho wa kuchukua fomu za kujiunga na mafunzo haya ni tarehe 18 JULAI 2014 saa sita kamili mchana.
Taasisi ya RafikiElimu Foundation kupitia MRADI WA WANAWAKE SALAMA
TANZANIA inatangaza nafasi za mafunzo ya UANDAAJI NA UTENGENEZAJI WA
VYAKULA-LISHE MAALUMU KWA WAGONJWA NA WENYE MATATIZO MBALIMBALI YA
KIAFYA.
KWA MAELEZO ZAIDI,WASILIANA NASI KWA SIMU NAMBA 0784406508
Au tuandikie kupitia barua pepe yetu :
rafikielimutanzania@gmail.com
0 comments:
Post a Comment