skip to main |
skip to sidebar
Kutokea kwa bomu lililo lipuka jana inalipotiwa kuwa Watu 10
wamefariki dunia na wengine zaidi ya 70 kujeruhiwa baada milipuko miwili
kutokea karibu na soko kubwa la nguo la Gikomba mjini Nairobi nchini
kenya.
Kuna uwezekano idadi hiyo ya watu waliofariki dunia ikaongezeka kutokana na hali ya baadhi ya majeruhi kuwa mbaya zaidi.
Milipuko
hiyo imetokea siku moja baada ya nchi za magharibi ikiwamo Uingereza
kuwataka raia wake wanaoishi nchini humo kurejea nyumbani kwa hofu ya
usalama.
Jeshi la polisi limesema kuwa linamshikilia mtu mmoja kwa
madai ya kuhusika kwenye tukio hilo na hakuna taarifa zaidi
zilizotolewa.
Msemaji wa Hospitali ya Kenyatta aliliambia Shirika la Habari la
AFP kuwa baadhi ya majeruhi waliopelekwa hospitalini hapo hali zao ni
mbaya.
Mfanyabiashara mmoja aliyekuwepo kwenye eneo la tukio alisema
kuwa alisikia mlio mkubwa uliofuatiwa na moshi uliotanda eneo lote la
soko na kwamba baada ya tukio hilo watu wengi walikimbia ovyo kuokoa
maisha yao.
“Watu wengi wamejeruhiwa. Sijui idadi ya watu waliopoteza maisha,
lakini kusema kweli mlipuko huu ni mkubwa na utakuwa umeleta madhara
makubwa,” alisema Mwangi Maina.
Hadi sasa hakuna kundi lililodai kuhusika na tukio hilo, lakini
wachunguzi wa mambo wanalitaja Kundi la Al-Shabaab kuwa huenda likawa
nyuma ya matukio hayo.
Kenya imekuwa ikiandamwa na matukio ya kigaidi
tangu ilipopeleka askari wake nchini Somalia kukabiliana na kundi lenye
msimamo mkali wa Kiislamu, Al-Shabaab.
Taarifa zilizotolewa na
vyombo vya habari vya nchi za magharibi zinasema kuwa zaidi ya watu 100
wamepoteza maisha katika kipindi cha miezi 18 iliyopita tangu Kenya
ianze kuandamwa na mashambulizi ya kigaidi.
Milipuko hiyo imekuja huku raia wengi wa kigeni waliokuwa nchini
Kenya kwa shughuli za utalii wakiwa wanarejea nyumbani kuitika wito
uliotolewa na serikali zao.
Tahadhari hiyo kutoka kwa Serikali ya
Uingereza ilieleza kuwa askari wa Al-Shabaab, huenda wakafanya
mashambulizi nchini Kenya katika muda wowote kuanzia sasa.
Taarifa hiyo iliwaonya raia wote wa Uingereza ambao wako nchini Kenya kwa shughuli ambazo siyo za dharura waondoke nchini humo.
Marekani, Ufaransa na Australia pia zimewataka raia wao walioko eneo la Pwani ya Kenya kuondoka mara moja.
Al-Shabaab
imeimarisha mashambulizi katika eneo hilo katika siku za hivi karibuni
huku likisisitiza kuwa linafanya hivyo kama njia ya kulipiza kisasi
kutokana na Kenya kupeleka majeshi yake nchini Somalia.
0 comments:
Post a Comment