skip to main |
skip to sidebar
From London With Love …!!! Star mkubwa wa filamu nchini Tanzania Wastara
Juma ambaye kwasasa yupo London Uingereza amevishwa pete ya uchumba
huko na mwanaume anayeonekana hapo pichani. Wastara aliweka picha kadhaa
kwenye akaunti zake za mitandao ya kijamii na wengine kudhani ni filamu
mpya. Star mwenzake pia Riyama Ally ambaye wapo wote huko London nae
aliandika “Ama kweli Mungu akitaka kukupa haandiki barua……, kila la
kheri mama huu mwanzo mzuri kwako”. Baada ya kuona picha hizo haraka
sana Swahiliworldplanet ilimuendea hewani Wastara akiwa huko huko London
na kumuuliza kama ni movie au ni kweli, tofauti na siku zote ambapo
kama ni movie Star huyo huweka kweupe lakini safari hii alionekana hana
la kusema pengine kwa furaha na kuishia kujibu kwa ufupi kwa kusema “No
comment” alipododoswa tena alijibu hivyo hivyo tena “No comment”.
Wastara Monalisa, Riyama Ally na Cloud ni takribani wiki tatu sasa wapo
London kwa mwaliko maalum na kucheza filamu inayoitwa Ughaibuni(Abroad)
ambapo tayari wameanza kuishuti. Tungependa kuwatakia kila la kheri
wawili hao .Angalia picha zaidi Wastara akivishwa pete hiyo.
0 comments:
Post a Comment