skip to main |
skip to sidebar
Inakuwaje mwanake wa miaka zaidi ya miaka 45 kupata mtoto ikiwa
katika masuala ya uzazi inasemekana kuwa mwanamke akifikisha umri wa
miaka zaidi ya 45 atakuwa hana uwezo wa kuzaa.
Kisha Mwanamke mmoja mkazi wa Kata ya Sindeni wilayani ya
handeni mkoa Tanga , Mwajuma Seif (50) amejifungua mtoto mwenye umbile
la ajabu hali iliyomtisha na kufikia hatua ya kuwaomba madaktari
wamfunge kizazi kwa kudai amechoka na anaogopa kubeba mimba zaidi.
Mtoto
huyo aliyezaliwa na umbile la ajabu aliweza kuishi kwa siku mbili tu
baada kuacha gumzo katika Mji wa Handeni na Mkoa wa Tanga kwa ujumla
kutokana na jinsi alivyokuwa.
Mwanamke huyo hadi sasa bado yupo wodini kutokana na hali yake
ya afya kutokuwa imara Mwajuma Seif alisema, awali alijua amebeba
ujauzito wa kawaida na hakuwa na wazo lolote kuwa inaweza kuwa ni mimba
ya mtoto wa ajabu ingawa alishangazwa na uzito wa mimba hiyo na kudhani
walikuwa watoto mapacha.
Pia Kaimu Mganga Mkuu na Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya
Handeni, Dk. Bakari Mdoe alisema tumbo la mama huyo liliwatia mashaka na
ndipowalipomuweka katika uangalizi maalumu hadi alipofikia muda wa
kujifungua.
0 comments:
Post a Comment